Header Ads

Niroge, imetajwa kuwania tuzo kubwa za kazi za ubunifu




KALI ZOTE BLOG



Image result for picha ya vanesa mdee






Wanasema hard work pays, lakini pia kilichogharamiliwa kinalipa zaidi.







Image result for picha ya vanesa mdee


video-vanessa-mdee-niroge
Video ya wimbo wa Vanessa Mdee, Niroge, imetajwa kuwania tuzo kubwa za kazi za ubunifu zinazojulikana kama Loeries za nchini Afrika Kusini.
Ni tuzo kubwa ambazo hushindanisha kazi mbalimbali za ubunifu kuanzia kwenye sekta zote za habari na mawasiliano. Niroge imetajwa kuwania kipengele cha video ya muziki.
“Our #Niroge video has been nominated for a #Loerie2016 ( Google Them ) in the Music Video category. Later on today we will find out if we win this prestigious award,” ameandika Vanessa kwenye Instagram.
Niroge iliongozwa na Justin Campos.
Kwenye kipengele hicho, pamoja na video zingine, Niroge inachuana na Everything ya rapper wa Nigeria, M.I, Jump ya Anatii, Cassper Nyovest na Nasty C na zingine.
Vipengele vya jumla kwenye tuzo hizo ni pamoja na Communication Design, Crafts – Print/Outdoor & Out of Home, Digital & Interactive Communication, Effective Creativity, Integrated Campaign, Live Events, Activations & Sponsorship, Media Innovation, Outdoor & Out of Home, PR Communication, Print Communication na Radio Communication.
Zingine ni Service Design, Shared Value, Student Awards na Television, Film and Video Communication

No comments