Video: Jah Prayzah asherehekea Watora Mari kufikisha views mil 1 ndani ya wiki 2
Jah Prayzah amesherehekea baada ya video ya wimbo wake wa ‘Watora Mari’ aliomshirikisha Diamond kufikisha views milioni moja kwenye mtandao wa Youtube.
Wimbo huo una wiki mbili tangu umewekwa kwenye mtandao huo August 12, mwaka huu lakini pia ndio wimbo wa kwanza wa msanii huyo kutazamwa mara nyingi kama hivyo.
Kupitia mtandao wa Instagram msanii huyo amewashukuru mashabiki wake kwa kuandika, “Thanks to all my fans out there,watora mari video with @diamondplatnumz has just reached a million views in a space of 2 weeks…”Aidha kwa mara ya kwanza wimbo huo utaanza kuchezwa leo kwenye runinga ya MTV Base.
Tazama video ya Jah Prayzah akisherehekea na rafiki zake kwa kufikisha views milioni moja.
Post a Comment