t!! POLISI PWANI WAPAMBANA NA MAJAMBAZI ZAIDI YA 10 ...ZAIDI YA DEFENDA 10 ZIPO ENEO LA TUKIO
Mapigano makali yanaendelea kati ya polisi na watu wanaosadikiwa kuwa ni majambazi eneo la Vikindu, wilaya ya Mkuranga, mkoa wa Pwani asubuhi hii.
Magari ya polisi (defenda) zaidi ya 16 yamefika eneo la tukio huku polisi wakiwa wameshika silaha zao kwa umakini mkubwa.
Kadhalika, magari yanayokwenda maeneo ya Vianzi Mkuranga, Malela, Pemba Mnazi, Mfuru yamefungwa kutokana na mapambano hayo.
Inadaiwa wamekamatwa majambazi 14 na wengi wao ni askari wastaafu. Inaelezwa kuwa viongozi wa wahalifu wao ni Kanali wa Jeshi mstaafu.
Pia tunaarifiwa kuwa kuna taarifa za vifo katika mapambano hayo...
Tutawaletea taarifa kamili hapa hapa
Post a Comment