Ubuyu: Gigy Money awataja mastaa 6 aliotoka nao kimapenzi
KALI ZOTE BLOG
Gigy Money Jumanne hii aliwaacha mdomo wazi mashabiki wake baada ya kuwataja live kwenye runinga mastaa 6 wakiume aliotoka nao kimapenzi.
Video queen huyo ambaye amewai kutamba katika video za mastaa mbalimbali wa bongo, amedai amewai kutoka kimapenzi na AliKiba, Abdu Kiba, Rich Mavoko, Harmonize, Hemed Phd pamoja na mtangazaji wa kipindi cha runinga cha Siz Kitaa cha Clouds TV, Casto Dickson ambaye alidai alikuwa tayari kumzalia mtoto.
“Nilikuwa na Casto mpaka nilikuwa tayari kumzalia,” Gigy Money alikiambia kipindi cha Take One cha Clouds TV. “kwa sababu anajua upendo kwa mtoto, lakini wakaja wanawake wamjini wakakorofisha, lakini hajawai kuniambia kama tumeachana, sijui kama tumeachana,”
Gigy ambaye pia ni mtangazaji wa Choice FM alidai Mama yake mzazi alimzaa nyuma ya mlango wa choo.
Pia alisema kwamba aliwahi kujitoa kimwili katika umri mdogo ilia pate hela ya kuweza kumnusuru mama yake mzazi kulipa deni la mkopo wa Benki
Post a Comment