Navy Kenzo: Ngoma yetu mpya ina hadhi ya kuingia kwenye chati za Billboard
KALI ZOTE BLOG
Kundi la wasanii wa Bongo Flava la Navy Kenzo linaloundwa na Nahreel na Aika, limesema single yao mpya ni shida!
Wamesema wimbo huo una vigezo vyote vya kuweza hata kuingia kwenye chati za Billboard.
“Tumekuwa tukifanya muziki mzuri na wa tofauti ili tuifikishe Bongo Flava mbali. Sasa kuna nyimbo inakuja watu wakae tayari kwa sababu tumewekeza sana kwenye production na kila kitu,” waliiambia XXL ya Clouds FM.
“Ni ngoma kali Sana kuanzia style na kila kitu. Pia album yetu ‘Above In a Minute’ inakuja na wnyimbo hiyo itakuwepo pia, tunataka tufanye vitu vikubwa ikiwemo kuzifikia chati za Billboard,” waliongeza
Post a Comment