Akana kwamba sehemu nyeti ilimzuia KULUKA
KALI ZOTE BL0G
Mrukaji wa Japan anayetumia mti kurukia Pole Vault Hiroki Ogita ameelezea kushangazwa kwake baada ya ripoti kusema kuwa sehemu yake nyeti ilimzuia kusonge mbele katika michezo ya Olimpiki ya Rio de Janeiro.
Kanda ya video ya mwanariadha huyo inayoonyesha kitu kama sehemu hiyo ikigonga ufito ilisambaa haraka katika mitandao ya kijamii.
Miguu yake ilikuwa tayari imeugonga ufito huo lakini mikono yake ikamalizia .
''Sikudhani kwmba vyombo vya habari vya kigeni vingeweza kunidhalilisha hivi'',alisema mwanariadha huyo wa miaka 28 katika mtandao wake wa Twitter.
''Si swala geni iwapo ni ukweli lakini ni swala la kuhuzunisha kwa kulifanyia mazaha jambo kama hili''.
Mtaalamu mmoja wa mchezo huo amesema kuwa tayari alikuwa ameugonga ufito huo kupitia mwili wake,alisema mkufunzi wa mchezo huo David Yeo kutoka Singapore.
''Nadhani ni kuanguka kwa ufito huo ndio kuligusa eneo hilo nyeti kwa bahati mbaya''.
Bwana Ogita hatahivyo aliuruka ufito huo katika jaribio lake la pili lakini akashindwa kuendelea baada ya kuruka urefu wa mita 5.45 pekee katika mruko wake wa mwisho.
Lakini mashabiki wake waliingia katika mitandao ya kijamii na kumpa matumaini kwamba mchezo huo hatahivyo haukuisha vibaya.
Na baada ya kutazama marejeleo ya kanda hiyo ya video yeye mwenye alifurahishwa na kilichokuwa kikiendelea upande wa mashabiki wake.
Post a Comment