SERIKALI YA JIPANGA KUTHIBITI UKIMWI
Serikali imepanga kusambaza bure kondomu milioni 21 nchini kuanzia Jumanne hii ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi.
Kaimu mkurugenzi katika mpango wa kuthibiti ukimwi, wizara ya afya, maendeleo ya jamii, jinsia, wazee na watoto, Eddah Katikiro ameyasema hayo Jumatatu hii alipokuwa akizungumzia maandalizi ya usambazaji wa kondomu hizo utakaofanyika kitaifa mkoani Mbeya.
Katikiro amesema kondomu hizo zitakuwa zinatolewa bure ili wananchi wazipate kwa kazi ya kuzuia VVU na kwenye uzazi wa mpango.
“Kondomu hizi zinatarajiwa kusambazwa kwa njia mbalimbali zikiwemo kupitia kwa ofisi za watendaji wa vijiji, kata, kwenye mabaa, mahoteli na mahali popote panapotolewa huduma za afya,” alisema.
Kwa upande wake afisa habari wa wizara hiyo, Shoko Subira alisema mpango huo unatekelezwa kutokana na kuwepo malengo ya kuthibiti maambukizi ya VVU ambapo mataifa mbalimbali yanataka yasiwepo ifikapo mwaka 2030.
Post a Comment