Mpiga tarumbeta wa Bob Marley, afariki
KALI ZOTE BLOG
Mpiga tarumbeta Headley Bennett, ambaye alishiriki katika wimbo wa kwanza wa mwanamuziki maarufu wa nyimbo za rege Bob Marley 'Judge Not,' amefariki akiwa na umri wa miaka 85.
Mwanawe Carol Bennett, alithibitisha kifo cha mwanamuziki huyo siku ya Jumapili.
Carol hakusema sababu maalum ya kifo cha mwanamuziki huyo, lakini alisema babake alikuwa akiugua shinikizo la damu na hivi majusi alipatika na saratani ya kiume.
Benneth alishiriki na wanamuziki wa nyimbo za rege kama vile Bunny Wailer na Gregory Isaacs.
Alituzwa na serikali ya Jamaica mwaka wa 2005 kama Mjamaica wa sita mwenye hadhi ya juu.
Post a Comment