Header Ads

zaidi ya saa moja na makahaba waishio nchini Italia ambao

PAPA Francis Kiongozi Mkuu wa kanisa Katoliki Duniani amekaa kwa zaidi ya saa moja na makahaba waishio nchini Italia ambao walisafirishwa kutoka nchi mbalimbali duniani zikiwemo za Afrika.
Papa mwenye umri wa miaka 79 amekua akikemea vitendo vya kusafirisha wanawake kutoka taifa moja kwenda lingine ili kuwatumikisha katika biashara za ngono.
Akiwa na wanawake 20 waishio katika moja ya jengo linalomilikiwa na Kanisa Katoliki katika Mji Mkuu wa Italia kiongozi huyo alizungumza na wanawake hao akitaka kujua namna walivyoingia biashara hiyo haramu.


Wanawake hao wenye umri unakadiriwa kuwa kati ya miaka 30 walitekwa na mwanamme mmoja. Miongoni mwao wapo wanaigeria saba, waromania sita na wanawake wanne kutoka Albania, huku wengine watatu katika kundi hilo wakitoka Italia, Tunisia na Ukraine.

Wanawake hao waliokolewa kutoka kwenye madanguro walikokuwa wametekwa na mwanamume aliyekua akiwauza kama makahaba na sasa wamepewa makazi na ulinzi katika jengo la ghorofa linalomilikiwa na kanisa katoliki katika mji mkuu wa Italia.


Aidha, wamekiri sababu kubwa inayopelekea kwenda huko kuwa ni ajira ambapo wafanyabiashara Italia na nchi nyingine kutoka mataifa ya Ulaya huwachukua kwa kuwaahidi kuwapa kazi na wakifika huko hulazimishwa kufanya ukahaba.

Wote pamoja walikua na umri wa takriban miaka 30 na ''walinyanyaswa sana kimwili'' na sasa wanaishi chini ya ulinzi, umesema uongozi wa Vatican.


Papa Francis amewatia moyo makahaba hao wenye nia ya kuachana na biashara hiyo, amewataka wawe “thabiti” wakati wanapoanza maisha mapya kwa usaidizi wa kituo cha Papa Yohana wa pili.

No comments