Mshukiwa wa ugaidi auawa kwa risasi Kigali, Rwanda
KALI ZOTE BLOG
Polisi nchini Rwanda wanasema wamemmpiga risasi na kumuua mtu mmoja anayeshukiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi mjini Kigali.
Tangazo lililotolewa na polisi ya nchi hiyo limesema kwamba jana usiku kumekuwa na ufyatulianaji risasi baina ya polisi waliokuwa wanamsaka mwanamume huyo aliyetambuliwa kama Channy Mbonigaba.
Afisa mmoja wa polisi alijeruhiwa kabla ya mshukiwa huyo kuuawa.
Mtu huyo ni wa pili kuuwawa na polisi nchini Rwanda mwaka huu kwa kupigwa risasi akituhumiwa kujihusisha na vitendo vya kigaidi hususani kushirikiana na kundi la Islamic State linalopigana nchini Syria.
Mwezi wa kwanza mwaka huu polisi walimuua Muhammed Mugemangano aliyekuwa anazuwilia katika kituo cha polisi kwa tuhuma za kusajili vijana na kueneza propaganda za kundi la Islamic State.
Tangu wakati huo, kundi la watu 23, wote Waislamu, walikamatwa na kufunguliwa mashitaka ya kujihusisha na kundi la Islamic State.
Wengi wao wanakana mashtaka hayo baadhi wakisema yalichochewa na Waislamu wenzao kutokana na mivutano ya kidini baina yao.
Kesi dhidi yao bado inaendelea.
SORCE BBC
Post a Comment