Header Ads

KABURI LA FUKULIWA KISHAPU MKKOANIA



Wananchi,viongozi wa serikali ya kijiji wakifukua kaburi la mtoto mwenye ualbino katika kijiji cha Bunambiyu wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga


Askari polisi akishiriki zoezi la kufukua kaburi la mtoto huyo
***

Habari kutoka Kishapu mkoani Shinyanga zinaarifu kuwa kaburi alilozikwa mtoto mwenye albinism Michael Juma mwenye umri wa miaka miwili na nusu, mkazi wa kijiji cha Bunambiyu kata ya Bunambiyu wilaya ya Kishapu aliyefariki dunia siku ya Jumamosi wiki iliyopita, limefukuliwa kisha kuzikwa tena.



Hatua ya mwili huo kufukuliwa imekuja baada ya kuibuka utata uliohusisha imani za kishirikina kwamba baadhi ya viungo vya mwili wa mtoto huo havipo.

Mwili wa mtoto huyo kwa mara ya kwanza ulizikwa siku ya Jumapili wiki iliyopita kisha kufukuliwa na kuzikwa upya siku ya Alhamis Agosti 18 mwaka huu baada ya Mahakama kutoa kibali mwili ufukuliwe ili kumaliza utata ulioibuka.


Akizungumza kabla ya kufukua mwili huo, katibu wa chama cha watu wenye ualbino mkoa wa Shinyanga Lazaro Anael amesema marehemu alizikwa akiwa na viungo vyake vyote vya mwili na wazazi ,viongozi wa kijiji na kata walijiridhisha kwa kuuona mwili na hakuna kiungo kilichokatwa.


Amesema cha kushangaza baada ya mazishi alipigiwa simu na mkurugenzi wa shirika la Under The Same Sun Vick Ntetema aliyekuwepo hata siku ya mazishi akimueleza kuwa kaburi la mtoto huyo linatakiwa kufukuliwa kwa madai kuwa kuna utata umejitokeza.

Mzazi wa marehemu Juma Masudi amesema mwanae alifariki Siku ya Jumamosi Agosti 13,2016 na kuzikwa Agosti 14 mwaka huu baada ya kuugua na hakuna kiungo cha mtoto kilichokatwa.

Baada ya kufukua kaburi hilo daktari Helena Kaunda kutoka kituo cha afya Bunambiyu alisema viungo vyote vya mwili viko sawa na hakuna kilichokatwa hivyo mwili wa marehemu ukazikwa tena.

No comments