Header Ads

Rais wa zamani Kenya Mwai Kibaki alazwa Afrika Kusini



Bw Kibaki
Image captionBw Kibaki aliongoza Kenya kati ya 2002 na 2013
Aliyekuwa Rais wa Kenya Mwai Kibaki, 84, amelazwa hospitalini nchini Afrika Kusini akipokea matibabu maalum baada ya kuugua mwishoni mwa wiki.
Kiongozi huyo wa zamani aliugua akiwa nyumbani kwake na akapelekwa hospitalini Karen, Nairobi Jumamosi jioni kabla ya kusafirishwa Afrika Kusini Jumapili.
"Aliandamana na daktari wake. Tunamtarajia arejee nyumbani hivi karibuni, na Wakenya watafahamishwa kuhusu hali yake wakati mwafaka," taarifa iliyotolewa na familia yake ilisema.
Desemba mwaka 2002, Bw Kibaki aliumia baada ya kuhusika katika ajali ya barabarani wakati wa kampeni na akapelekwa Uingereza kwa matibabu.
Aliapishwa kuwa rais muhula wake wa kwanza akiwa kwenye kiti cha magurudumu.
Bw Kibaki na mkewe LucyImage copyrightAFP
Image captionBw Kibaki na mkewe Lucy
Mkewe, Lucy Muthoni Kibaki, alifariki Aprili mwaka huu akitibiwa jijini London

No comments