Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amezua utata mwengine
KALI ZOTE BLOG
Mgombea wa urais kupitia chama cha Republican nchini Marekani Donald Trump amezua utata mwengine kwa kuwataka wafuasi wake wanaomiliki bunduki kumzuia mpinzani wake Hillary Clinton kuwanyima haki zao za kikatiba.
Miongoni mwa habari nyingine kuu leo, Donald Trump amezua tena utata baada ya kuonekana kuwataka wafuasi wake wenye bunduki wamzuie Clinton na Serena Williams ameshindwa tena Rio.
1. Trump azua utata tena Marekani
Hata hivyo kampeni ya Bi Clinton imeshtumu matamshi hayo ikisema ni ya hatari.
2. Unyanyasaji wa watoto Nauru, Australia
Maelezo yamechapishwa kuhusu kile kinachotajwa kuwa kuenea kwa unyanyasaji wa watoto wanaozuiliwa katika kituo kimoja nchini Australia katikati ya kisiwa cha Pasifiki cha Nauru.
Gazeti la The Guardian, linasema kuwa zaidi ya ripoti 2000 zilizofichuliwa zinaonyesha picha mbaya za ukatili, unaohusisha unyanyasaji wa kingono, kupigwa, na jaribio la kujitoa uhai miongoni mwa vijana wanaotafuta hifadhi.
3. Panama kuwasaidia wahamiaji kutoka Cuba
Taifa la Panama limeahidi kuwasaidia maelfu ya wahamiaji kutoka Haiti na Cuba ambao wameingia nchini humo kutoka Colombia wakijaribu kufika Marekani.
Rais Yuan Carlos Varela amesema serikali yake itawasaidia kuendelea na safari yao,licha ya msimamo wake mkali dhidi ya wahamiaji haramu.
4. Wasiwasi wa ghasia uchaguzini Zambia
Mkuu wa tume ya uchaguzi nchini Zambia ameelezea kiwango cha juu cha ghasia nchini humo kabla ya uchaguzi mkuu hapo kesho, kuwa kitu ambacho hakijawahi kuonekana.
Esau Chulu amewataka viongozi wa chama cha tawala cha PF na wenzao wa chama pinzani cha UPND kuwadhibiti wafuasi wao.
5. UN yahimiza kusitishwa kwa vita Aleppo
Umoja wa mataifa umetoa wito wa kusitishwa mara moja kwa vita katika mji wa pili kwa ukubwa nchini Syria, Allepo.
Unasema kuwa mapigano makali yamewaacha zaidi ya watu milioni mbili bila maji na umeme.
Vyombo vya habari vya serikali ya Syria vinasema kuwa wanajeshi wa serikali wameyakomboa baadhi ya maeneo.
6. Serena Williams ashindwa tena Rio
Na hatimaye bingwa mtetezi wa mchezo wa tenisi upande wa wanawake Serena Williams ambaye pia anaorodheshwa nambari moja duniani ameondolewa na mchezaji wa Ukraine Elina Svitlina katika michezo ya Olimpiki inayoendelea mjini Rio de Janeiro nchini Brazil.
Post a Comment