Rooney atangaza kuacha soka la kimataifa mwaka 2018
KALI ZOTE BLOG
Mshambuliaji nyota na nahodha wa Uingereza Wayne Rooney anatarajia kustaafu soka la kimataifa baada ya kumalizika kwa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2018 itakayofanyika nchini Urusi.
Nyota huyo wa Manchester United alikuwa akizungumza na wanahabari kwa mara ya kwanza toka kocha mpya wa timu ya taifa ya Uingereza sam Allardyce athibitishe kuwa ataendelea kuwa nahodha.
Akihojiwa Rooney ambaye amefunga mabao 53 katika mechi 115 kwa Uingereza, amesema pindi Kombe la Dunia la Urusi litakapomalizika anadhani wakati wake wa kuaga soka la kimataifa utakuwa umefika.
Nyota huyo aliendelea kudai kuwa michuano hiyo itakuwa nafasi yake ya mwisho kufanya kila kitu na Uingereza hivyo bado ataendelea kufurahia miaka miwili iliyobakia.
Kama Rooney akicheza mchezo wa Jumapili hii wa kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Slovakia, atakuwa amevunja rekodi ya David Beckham ya kucheza mechi nyingi katika timu ya taifa.
Post a Comment