Header Ads

Mhubiri mpinga mapenzi ya jinsia moja akimbia mafuriko Marekani


Nyumbani kwa Tony PerkinsImage copyrightTONY PERKINS / FACEBOOK
Mhubiri anayepinga mapenzi ya jinsia moja Tony Perkins pamoja na familia yake, wamelazimika kukimbia kutoka nyumbani kwao Louisiana kutokana na mafuriko.
Perkins, ambaye huamini majanga ya kiasili hutumwa na Mungu kama adhabu kwa wapenzi wa jinsia moja, alitoroka nyumbani akitumia mtumbwi.
Mwaka 2015, alizua utata baada ya kusema anakubaliana na kauli kwamba majanga hutumwa na Mungu kwa sababu ya utoaji mimba na ndoa za wapenzi wa jinsia moja.
Bw Perkins amefichua kwamba amelazimika kutoroka nyumbani kwake kutokana na mafuriko.
Aidha, amesambaza picha kwenye Facebook kuonesha hali ilivyokuwa na pia akapakia mtandaoni kanda ya sauti akisimulia yaliyojiri.
"Haya ni mafuriko yanayokaribia kiwango kinachosimuliwa kwenye Biblia," amesema kwenye mahojiano na Family Research Council.
Tony PerkinsImage copyrightGOOGLE
Image captionTony Perkins aliwania kiti cha useneta Marekani mwaka 2002 na kwenye kampeni alipinga haki za wapenzi wa jinsia moja
Shirika la Msalaba Mwekundu limesema mafuriko ya Louisiana ndilo janga mbaya zaidi kukumba Marekani tangu kutokea kwa kimbunga cha Hurricane mwaka 2012.

No comments