Rio 2016: Kamati ya Olimpiki Kenya yavunjiliwa mbali
KALI ZOTE BLOG
Waziri wa michezo nchini Kenya Hassan Wario ametangaza kuvunjilia mbali Kamati ya Taifa ya Olimpiki kuhusiana na maandalizi ya timu hiyo kwa michezo ya Olimpiki iliyomalizika majuzi mjini Rio de Janeiro, Brazil.
Waziri ametangaza hatua hiyo kwenye kikao na wanahabari huku ikibainika kwamba bado kuna wachezaji ambao hawajaondoka Rio.
Miongoni mwao ni mbunge Wesley Korir, aliyeshiriki mbio za Marathon, ambaye amesema wanaishi katika hali duni.
Bw Wario amesema majukumu ya kamati hiyo, maarufu kama NOCK, yatatekelezwa na Sports Kenya.
Waziri huyo pia ameunda kamati ya kuchunguza yaliyojiri wakati wa maandalizi ya michezo hiyo na wakati wa michezo yenyewe.
Kundi hilo linafaa kuwasilisha ripoti Septemba 30.
Post a Comment