Swansea yakata dau la Everton
Timu ya soka ya Swansea City imekataa dau la pauni milioni 10 lilitolewa na Everton ili kuweza kumsajili beki Ashley Williams.
Taarifa zinasema beki huyo raia wa Wales ambae pia ni nahodha wa Swansea alikua anakaribia kufika makubaliano ya mwisho kwenda Goodison Park kujiunga na Everton.
Williams ambae atafikisha miaka 32 mwezi huu anamkataba na timu yake unaomalizika mwaka 2018, msemaji wa klabu hiyo anasema hawako tayari kumuuza beki huyo.
Beki huyo ameichezea timu yake zaidi ya michezo 300 alisajiliwa kwa kiasi cha pauni 300,000 toka klabu ya Stockport mwaka 2008.
Everton wanasaka saini ya beki huyu ili kwenda kuziba pengo litakaloachawa na mlinzi wao mahiri John Stones anayehusishwa kutaka kujiunga na matajiri wa Man City.
Post a Comment