Header Ads

Taufatofua, mchezaji aliyesisimua kwa mavazi Rio

KALI ZOTE BLOG


Pita Nikolas TaufatofuaImage copyrightALL SPORT/GETTY IMAGES
Image captionPita Nikolas Taufatofua ni mwanataekwondo
Wakati wa sherehe za ufunguzi wa Michezo ya Olimpiki mjini Rio de Janeiro nchini Brazil Ijumaa, kulikuwa na wachezaji 207 waliobeba bendera za mataifa yao.
Lakini mmoja alionekana kuwasisimua watazamaji zaidi ya wengine.
Alikuwa ni Pita Nikolas Taufatofua, mwanamichezo kutoka Tonda ambaye alikuwa kifua wazi na chini amevalia vazi la kitamaduni la Tonga, kwa jina ta'ovala.
Taufatofua, alizaliwa Australia lakini akalelewa Tonga.
Ndiye mchezaji wa kwanza kutoka Tonga kuwakilisha taifa hilo katika mchezo wa taekwondo. Yeye huishi Brisbane ambapo huwasaidia watoto wasio na makao.
Kwa mujibu wa tovuti ya USA Today, mwanataekwondo huyo wa umri wa miaka 32 alijaribu kufuzu kwa Olimpiki mara mbili awali.
Pita Nikolas TaufatofuaImage copyrightREUTERS
Image captionPita Nikolas Taufatofua
Atashindana katika kitengo cha wanaume wa uzani wa kilo 80 na zaidi Jumamosi tarehe 20 Agosti.
Ni mmoja kati ya wachezaji saba wanaowakilisha taifa hilo la Polynesia linalotawaliwa na ufalme katika Michezo ya Rio.
Tonga imeshinda nishani moja pekee katika historia yake, medali ya fedha mwaka 1996.
TongaImage copyrightLEON NEAL/AFP
Image captionMbeba bendera huyu wa Tonga alisisimua wengi kwa kifua chake wazi kilichong'aa kutokana na mafuta

No comments