Al-Shabab washambulia kambi la majeshi l la nchini Kenya nchini Somalia
Kundi la al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.
Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.
"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.
Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.
Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."
Post a Comment