Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi katika Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya usafi wa Mazingira
Jumuiya ya vijana wa Chama cha Mapinduzi CCM kata ya Ndembezi
katika Wilaya ya Shinyanga Mjini imefanya usafi wa Mazingira katika kituo cha
afya cha Ngokolo Mjini Shinyanga,ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka
arobaini ya Chama hicho ambapo kilele chake ni Februari 05,mwaka huu.
Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana wa ccm-uvccm kata ya Ndembezi DOTTO
JOSHUA amesema maadhimisho ya Chama
hicho kwa mwaka huu 2017 yatafanyika kwa utaratibu wa kufanya shughuli
mbalimbali za kijamii ikiwemo usafi,badala ya mikutano,ngoma na Maandamano kama
ilivyozoeleka.
Mwenyekiti huyo amesema Miaka arobaini tangu kuzaliwa kwa
Chama cha Mapinduzi CCM, wananchi wameendelea kuwa na imani na Chama hicho tawala ambacho kimepiga
hatua mbalimbali za mafanikio.
Katibu wa Chama cha Mapinduzi CCM wilaya ya Shinyanga mjini CHARLES SANGURA amesema kuelekea kilele cha maadhimisho hayo
Chama na Jumuiya zake,ikiwemo wazazi,UWT,na vijana watafanya shughuli mbali mbali za kijamii
ikiwemo utoaji wa Elimu, usafi wa mazingira, na upandaji wa miti.
Post a Comment