Header Ads

Mjumbe wa Kamati kuu Chadema, Edward Lowassa amesema njia ya kuingia Ikulu 2020 ni nyeupe


Image result for picha ya lowassa
Mjumbe wa Kamati kuu Chadema, Edward Lowassa amesema njia ya kuingia Ikulu 2020 ni nyeupe katika uchaguzi mkuu utakaofanyika mwaka huo huku akitaka wananchi kujitokeza kupiga kura.
Lowassa ameyasema hayo Kahama, kijiji cha Mseki nyumbani kwa Kada wa Chadema, James Lambeli. Alisema anashindwa kuongea na wananchi wa kijiji hicho kwa kuhofia kukamatwa na polisi kama alivyofanyiwa Geita na kuwataka wananchi kuwa wavumilivu mpaka itakapofika 2020.
Alisema,” Kuweni wavumilivu hadi itakapofika 2020 mjitokeze kupiga kura kama ntakuwa hai, ntagombea tena urais kupitia muungano wa vyama pinzani.”
Edward Lowassa aligombea urais mwaka 2015 lakini alishindwa na Rais John Pombe Magufuli.

KUWA WAKWANZA KUWA KARIBU NA SYLAS DENNIS KUPATA HABARI ,MATUKIO

No comments