Header Ads

Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, makala ya 31, itang'oa nanga Jumamosi 14 Januari

  • 7
Ivory CoastHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Michuano ya Kombe la Mataifa Afrika, makala ya 31, itang'oa nanga Jumamosi 14 Januari pale wenyeji watakapokabiliana na Guinea-Bissau ambao wanashiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza.
Kwa baadhi ya mashabiki, hii ni michuano tu ya kawaida ya soka.
Lakini AFCON kwa sasa ni michuano yenye ushindani mkali na yenye wachezaji nyota kama vile Riyad Mahrez, Sadio Mane na Pierre-Emerick Aubameyang.
Ivory CoastHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionYaya Toure akiwa ameinua kikombe 2015
Michuano hii inapong'oa nanga, tunaangalia matukio muhimu ya furaha na ya kusikitisha pia ambayo hayasahauliki katika historia ya AFCON.
1994: Zambia yajikwamua baada ya mauti
ZambiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Mnamo 27 Aprili 1993, timu ya taifa ya Zambia ilikuwa safarini mechi ya kufuzu Kombe la Dunia nchini Senegal ndege iliyowabeba ilipoanguka na kutumbukia baharini mita 500 kutoka mji wa Libreville, Gabon.
Abiria wote 25 waliangamia pamoja na wahudumu watano.
Mwaka mmoja baadaye, Zambia ilijijenga na kufana sana michuano ya Kombe la Mataifa Bingwa Afrika 1994. Walifika fainali ingawa walishindwa na Nigeria 2-1.

2012: Herve Renard asaidia Zambia kutwaa kombe

ZambiaHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Herve Renard and Zambia win the Africa Cup of Nations in 2012Getty Images
Zambia walikosa ushindi fainali 1994 lakini walifanikiwa 2012 chini ya kocha wao Mfaransa Herve Renard ambapo walikabiliana na Ivory Coast fainali.
Kwenye mechi hiyo, kulipigwa mikwaju 18 ya penalti, na Zambia wakashinda 8-7.

No comments