watu mamilioni wako katika hatari ya kupoteza maisha
Umoja wa Mataifa umesema mamilioni ya watu wako katika hatari ya kupoteza maisha kutokana na athari za kiangazi na ukame nchini ETHIOPIA.
Mkuu wa Ofisi ya Msaada wa Kibinadamu ya Umoja wa Mataifa, STEPHEN O'BRIEN amesema ukame huo umesababisha watu milioni 5.6 nchini ETHIOPIA kuhitaji msaada wa dharura
O'BRIEN amehadharisha kuwa iwapo hatua za dharura hazitachukuliwa watu wengi watapoteza maisha kutokana na njaa kama ilivyokuwa mwaka jana.
Mkuu wa Kitengo cha Kukabiliana na Majanga nchini ETHIOPIA, MITIKU KASSA amesema nchi hiyo inahitaji msaada wa dola milioni 948 za Marekani ili iweze kukabiliana na hali ya ukame na baa la njaa.
Post a Comment