Header Ads

Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kumkamata





Jeshi la Polisi Mkoa wa Shinyanga 
kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kumkamata  Msichana mmoja mkazi wa mtaa na kata ya
kitangili katika
  Manispaa ya Shinyanga
kwa tuhuma za kutumbukiza mtoto chooni.

Msichana huyo aliyetajwa kwa Jina la NEEMA JAPHET mwenye umri wa miaka 23,anatuhumiwa kumtumbukiza
chooni mtoto wake mwenye umri wa siku moja,Januari 20,mwaka huu.

Kaimu kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa  wa Shinyanga Elias Mwita amesema kufuatia uchunguzi
kati ya majirani, serikali ya  mtaa huo,
kwa kushirikiana na Polisi   mtuhumiwa
huyo  alikamatwa  Jana Januari 24, majira ya saa tatu asubuhi,akiwa
chumbani kwake katika nyumba anayoishi.

Kaimu kamanda huyo amesema baada ya mtuhumiwa kukamatwa amekiri
kuhusika na tukio hilo kwa maelezo kuwa mtoto wake alitumbukia kwenye tundu kwa
bahati mbaya wakati akijisaidia

Tukio hilo  lilitokea
Januari 20,majira ya saa kumi na moja Jioni,wakati waumini wa kanisa la AICT
Kitangili walipobaini mtoto kutumbukizwa chooni,baada ya kusikia sauti ya kilio
kutoka kwenye  tundu la choo.

kuwa wakwanza kupata hii kutoka kwa Christian Bella ft Khaligraph Jones Ollah  Official Music Video

No comments