WANANCHI WASHINYANGA KUSHIRIKI MAADHIMISHO YA SHERIA
Wakazi wa mji wa Shinyanga na maeneo yaliyopo Jirani wameombwa kushiriki kwenye maadhimisho ya wiki ya Sheria nchini ili waweze kujifunza na kupata ushauri mbalimbali kuhusu masuala ya kisheria.
Akizindua wiki ya sheria kaimu mkuu wa mkoa wa Shinyanga,Fadhiri Nkulu ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Kahama amesema maadhimisho hayo ni fursa kwa wananchi kujua sheria,hivyo ni jukumu la wadau wa masuala ya kisheria ikiwemo mahakama kubainisha hatua zilizofikiwa katika uboreshaji wa huduma,hivyo Jamii inapaswa kuhudhuria ili kujifunza
Ameonya mahakimu wanaokiuka maadili ya kazi kwa kujihusisha na vitendo vya rushwa,hivyo kuminya upatikanaji wa haki na kuchafua sifa ya mhimili wa mahakama,kwamba mamlaka husika hazitosita kuchukua hatua za kinidhamu.
Kwa upande wao Baadhi ya wananchi waliokuwa wamehudhuria katika uzinduzi wa wiki ya sheria wamesema hawana uelewa wa kutosha hivyo kuimba idara ya mahakama na wadau wengine kutoa elimu mara kwa mara kuhusu masuala ya kisheria,badala ya kusubiri maahimisho.
Kilele cha wiki ya sheria ni Februari mbili,mwaka huu ambapo uzinduzi kimkoa umefanyika leo katika viwanja vya kikosi cha zimamoto,huku kauli mbiu ya maadhimisho hayo kwa mwaka huu ikisema ‘’umuhimu wa utoaji haki kwa wakati,na kuwezesha ukuaji wa uchumi’’.
ANGLIA VIDEO YA HISTORIA YA SIMBA NA YANGA
Post a Comment