Header Ads

VIDEO: Tunisia wamefuzu robo fainali


Michezo ya Kundi B ya michuano ya AFCON 2017 imeendelea usiku wa January 23 2017 kwa michezo miwili kuchezwa, timu ya taifa ya Tunisia ambayo ilikuwa inahitaji ushindi ili kusonga mbele ilicheza dhidi ya Zimbabwe katika uwanja wa Stade de Amitie mjini Libreville.
Kundi B lilikuwa nne na timu pekee iliyokuwa imejihakikishia safari ilikuwa ni Senegal, lakini timu za ZimbabweTunisia na Algeria zote zilikuwa zinategemea matokeo ya mechi za leo ilikujua kama watafuzu au ndio safari yao imeishia hapo.
Kufuatia ushindi wa Tunisia wa 4-2 unawafanya wafuzu kucheza hatua ya robo fainali wakiungana na Senegal ambao ni vinara wa Kundi B, magoli ya Tunisia yakifungwa na Naimu Sliti dakika ya 9, Youssef Msakni dakika ya 22, Taha Khenissi dakika ya 36 na Wahbi Khazri dakika ya 44, wakati magoli ya Zimbabwe yamefungwa na Knowledge Musona dakika ya 43 na Tendai Ndoro dakika ya 58.



No comments