SERIKALI inazikumbusha taasisi zote zenye leseni za mawasiliano zilizotolewa kabla ya Julai mosi
SERIKALI inazikumbusha taasisi zote zenye leseni za mawasiliano zilizotolewa kabla ya Julai mosi mwaka huu, kujisajili katika soko la hisa na dhamana kama sheria inavyoelekeza, vinginevyo zitaadhibiwa ikiwa ni pamoja na kusitishiwa leseni zao.
Imeelezwa kuwa kushindwa kutimiza sharti la usajili katika soko la hisa na dhamana ni kosa, hivyo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), na taasisi hizo zinatakiwa kukubaliana kwa maandishi kusitisha leseni za watakaoshindwa kukidhi matakwa kwa mujibu wa sheria.
Ukomo wa kujisajili uliowekwa unaishia Desemba 31, mwaka huu kwa kuzingatia sheria ya soko la hisa na dhamana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa alisema jana alipokuwa akitoa taarifa kwa umma kuhusu utekelezaji wa Sheria ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) kulingana na mabadiliko yaliyofanywa katika Sheria ya Fedha Namba 2 ya Mwaka 2016.
Alisema lengo la taarifa hiyo ni kuwapelekea ujumbe watoa huduma kuwa wana siku chache hivyo wahakikishe wanakamilisha mchakato huo.
Kwa mujibu wa Mbarawa, leseni hizo zinahusu miundombinu ya mawasiliano, huduma za mawasiliano na huduma za matumizi ambapo wamiliki wake wanatakiwa kuwa na umiliki wa Watanzania usiopungua asilimia 25 ya hisa zote kwa kipindi chote cha leseni.
“Kiasi cha hisa zisizopungua asilimia 25 kitapatikana kupitia soko la hisa na dhamana kadri ya sheria ya soko la hisa na dhamana la tanzania,” alisema.
Alisisitiza kuwa watakaopata leseni baada ya Julai mosi, mwaka huu, watatakiwa kutimiza sharti hilo katika kipindi kisichozidi miaka miwili tangu kupewa leseni.
“Kufuatia maelekezo hayo hapo juu napenda kuwakumbusha wenye kampuni zote zenye leseni za mawasiliano zinazotalewa kusajili kwenye soko la hisa na dhamana asilimia 25 kabla ya mwisho wa Desemba 2016, kufanya hivyo ili kutimiza matakwa ya
Post a Comment