CHAMA CHA DEMOKRASIA NA
MAENDELEO KIMEAHIDI KUTOA MSAADA WA MIFUKO MIA MOJA YA SARUJI KWA WAHANGA WA MAAFA
YALIYOSABABISHWA NA MVUA KUBWA ILIYONYESHA KATIKA MANISPAA YA SHINYANGA KATA YA
KITANGILI NA KUSABABISHA WANANCHI WALIO
WENGI KUKOSA MAKAZI.
HAYO YAMEJILI MAPEMA
LEO AMBAPO WAZIRI MKUU MSTAAFU AMBAYE PIA KADA WA CHAMA HICHO FREDRICK SUMAYE
AMEWAOMBA VIONGOZI WA SERIKALI KUACHA TABIA YA KUWAKEJELI WANANCHI WANAPOPATA
MATATIZO AMBAPO AMESEMA KUWA MISAADA YOTE INAYOTOLEWA NI KWAAJILI YA WANANCHI
WALIOPATWA NA MATATIZO HAYO
MWENYEKITI WABARAZA LA WANAWAKE CHADEMA AMBAYE PIA NI
MBUNGE JIMBO LA KAWE HALIMA MDEE AMEITAKA SERIKALI KUPITIA BAJETI YA MAAFA
KUWEZA KUSAIDIA AMBAPO PIA AMEAHIDI KUTOA MAGUNIA KUMI YA MCHELE KAMA CHAKULA
KWA WAHANGA.
AWALI AKISOMA RISALA
FUPI MWENYEKITI WA MAENDELEO KATA YA KITANGILI HAMIS OMARY AMEAINISHA MAENEO
YALIYOATHIRIKA NI KATA YA KITANGILI, KATA YA KIZUMBI NA KATA YA IBADAKULI
AMBAPO TAKRIBANI WATU 69 MAKAZI YAO YAMEHARIBIWA, NYUMBA 187 ZIMEEZULIWA PAA NA
KUTA KUBOMOLEWA NA UHARIBIFU WA MALI NA CHAKULA.
Post a Comment