kuepusha matukio ya kutupwa watoto
zimeshauri kutoa adhabu stahiki kwa wanaume wanaobainika kutelekeza watoto au wanawake wenye ujauzito wao,ili kuepusha matukio ya utoaji wa mimba,kuuawa,kutupwa na kutelekezwa watoto hasa wachanga..
Mkurugenzi wa Shirika la AGAPE JOHN MYOLA amesema ili kuepusha matukio ya kutupwa watoto,mamlaka hizo ikiwemo Polisi,Mahakama, na Ustawi wa Jamii zina wajibu wa kupokea, kusikiliza,na kuwasaidia wanawake waliotelekezewa mimba au watoto,badala ya kuwapuuza.
Hata hivyo amewaomba wasichana na wanawake kutochukua maamuzi magumu ya kutoa mimba au kuua watoto kwa sababu ya kutelekezwa,na badala yake wanapaswa kuwa wawazi ili waweze kupatiwa ushauri nasaha
Mkurugenzi huyo wa shirika la AGAPE ameshauri watoto wa kike kutokatishwa tamaa na badala yake wanapaswa kujitambua,na kufahamu kuwa wana thamani kubwa katika Jamii kwani wanategemewa kulitumikia Taifa.
Post a Comment