VIDEO: Gari lilivyochomwa moto NA WATU WANAOMPINGA Donald Trump
Wanasema haijawahi kutokea fujo za namna hii kwenye historia ya Marais wapya Marekani, hii imetokea kwenye mji wa Washington DC. wakati huu ambao Rais Donald Trump ameapishwa kuwa Rais wa 45 wa Marekani.
Waandamanaji wanaompinga waliandamana kwa wingi kwenye mitaa mbalimbali ya mji huo wakiwa na Mabango na wakipaza sauti kuonyesha wazi kwamba hawamtaki na wengine walivunja vioo vya Maduka, Magari na hata kuchoma moto gari moja la kifahari.
Katika kuonyesha kwamba hawaogopi Waandamanaji hao walivunja mpaka kioo cha gari la Polisi lililopita katikati yao kama inavyoonekana kwenye hii video hapa chini, inasemekana hadi sasa ni zaidi ya Waandamanaji 100 wamekamatwa na Polisi.
Post a Comment