Watu zaidi ya 20 wamefariki kutokana na baridi kali
Watu zaidi ya 20 wamefariki kutokana na baridi kali ambayo imeendelea kukumba maeneo mengi ya Ulaya.
Watu kumi walifariki kutokana na baridi hiyo kali Poland siku ya Jumapili.
Miili ya wahamiaji watatu, wawili kutoka Iraq na mmoja kutoka Somalia, ilipatikana karibu na mpaka wa Uturuki na Bulgaria.
Vifo pia vimeripotiwa Italia, Jamhuri ya Czech na Ukraine.
Safari nyingi za ndege pia zimesitishwa kutokana na hali mbaya ya hewa.
Nchini Uturuki, mlango wa bahari wa Bosphorus umefungwa na meli haziruhusiwi kupita kutokana na dhoruba kali ya theluji.
CHANZO BBC
Post a Comment