MICHEZO VIDEO:Goli moja la Himid Mao liloipa Azam FC kombe la Mapinduzi , Full Time 1-0
Bao la kiungo mkabaji na mwenye nidhamu ya kuchomekea muda wote Himid Mao limeipa Azam FC taji la tatu la Michuano ya Kombe la Mapinduzi Cup 2017 baada ya kupiga Simba 1G.
Mao alifunga bao hilo baada ya kupiga nyundo ya Moja kwa moja mita 18 na kumuacha Daniel Agyei hana la kufanya dakika ya 12 kipindi cha kwanza na kuwainua mashabiki wa Azam waliokuwa wamefurika uwanja wa Amaan Zanzibar.
Baada ya kufungwa bao hilo Simba walicharuka na katika dakika ya 27 beki Abdi Banda alimanusura aisawazishie Simba bao baada ya kupiga faulo ambayo ilimfanya mlinda mlango wa Azam Aishi Manula afanye kazi ya ziada na kuokoa hatari hiyo hadi dakika 45 kipindi cha kwanza Azam walikuwa mbele.
Kipindi cha pili kilikuwa kigumu kwa pande zote mbili huku kila timu ikifanya mabadiliko hata hivyo mabadiliko hayo hayakuweza kuisaidia Simba na kukubali kichapo cha goli 1-0.
Kwa matokeo hayo Azam Fc imeweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kuzifunga Simba na Yanga na kuweza kutwaa taji bila kufunga hata goli moja.
Goli la Azam FC lilifungwa katika dakika ya 12′ kupitia kwa Himid Mao goli ambalo lilidumu mpaka mwisho wa mchezo na hivyo kuifanya Azam FC kuibuka washindi wa kombe la Mapinduzi 2017.
Post a Comment