jenifa na patrick si watoto tena
jenifa
jenifa na patrick
Watu wengi watawakumbuka Jennifer na Patrick kwa jinsi walivyoweza
kutikisa tansia ya filamu Tanzania kipindi cha nyuma walipoibuliwa na
marehemu Steven Kanumba.
Watoto hawa wawili walicheza kwa ustadi mkubwa katika filamu za Uncle JJ na This is It zote za marehemu Kanumba.
Kwa sasa Hanifa Daud ‘Jennifer’ na Othman Njaidi ‘Patrick’ si watoto
tena. Wawili hawa hawajaonekana sana kwenye filamu baada ya Steven
Kanumba aliyewatoa kufariki.
Jennifer ambaye amehitimu kidato cha nne mwaka jana mara ya mwisho
alionekana kwenye filamu ya Zena na Betina ya Salma Jabu a.k.a Nisha
mwaka 2014. Kwa upande wake Patrick, yeye alisema kuwa hana shauku ya
kuigiza tena kama ilivyokuwa awali.
filamu ya Zena na Betina jenifa aliyoonekana 2014
jenifa
Credit: Bongo5
Post a Comment