Serikali nnchini Ivory Coast inaendelea kufanya mashauriano na wanajeshi
Serikali nnchini Ivory Coast inaendelea
kufanya mashauriano na wanajeshi nchini humo, ambao walifanya maandamano
katika miji mbalimbali nchini humo.
Mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe yalimalizika miaka kadhaa iliyopita lakini Serikali ingali ina
changamoto kubwa kuuunganisha taifa hilo ambalo lingali lina dalili za
utengano baada ya mapigano ya muda mrefu.
Waasi walishambulia
mwanzo katika mji wa katikati mwa nchi wa Bouake. Mbunge wa aneo hilo
anasema kuwa wanajeshi hao wanataka wapewe Dola 8,000 na nyumba kwa kila
mmoja wao.
Wanajeshi pia walifanya maandamano katika Korhogo, Daloa, Daoukro na Odienne.
Karibu
wote walioasi ni wale waliokuwa waas
i wa kundi la Forces Nouvell,
lililosimamia Kaskazini mwa nchi hadi mwisho wa mapigano ya wenyewe kwa
wenyewe mwaka 2011.
Walishirikishwa katika jeshi lakini wanasema
kuwa wangali wanaidai Serikali kiwango fulani cha pesa cha ule muda
waliokuwa waasi.
Serikali ililazimika kulipa pesa chini ya mpango
kama huu na kwa sasa imejikuta katika hali ya kutafuta pesa zingine kama
hizi ili kuwalipa wahusika.
Post a Comment