Header Ads

Senegal na Liverpool, Salif Diao ameiambia timu yake ya zamani kwamba inapaswa kumsaidia Sadio Mane


Senegal
Image captionSadio Mane

Mchezaji wa zamani na kiungo wa timu za Senegal na Liverpool, Salif Diao ameiambia timu yake ya zamani kwamba inapaswa kumsaidia Sadio Mane kurejea katika hali yake ya kawaida baada ya kukosa mkwaju wa adhabu ambao uliisababishia timu yake ya Senegal kuondolewa katika michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika nchini Gabon.
Mane alivunjika moyo baada ya kukosa penalti muhimu katika robo fainali dhidi ya mahasimu wao timu ya Cameroon.Diao amesema kwamba kuna haja ya kuwa na mtazamo chanya juu ya kushindwa kwa timu ya Senegal na siyo kumfanya Mane kuwa ndiye mchawi wao.
Ilikuwa ni huzuni kuu kwa kilichomtokea. Ni kawaida barani afrika kumtafuta mchawi lakini nadhani amecheza vizuri ukiondoa kasoro hiyo, pengine tulitarajia makubwa ziaidi kutoka kwake na timu nzima lakini nafikiri bado hajakomaa sawasawa.
Ingawa naamini akisalia na timu ya Liverpool kwa miaka miwili zaidi,anaweza kuwa bora zaidi na kubeba jahazi la timu, ameyasema hayo Diao ambaye alikuwa sehemu ya timu ya Senegal ambayo ilipoteza mchezo dhidi ya Cameroon katika michuano ya fainali za mwaka 2002 kombe la mataifa ya Afrika mtanange uliosambazwa nchini Mali.
Pamoja na kupoteza nafasi ya kusonga mbele katika michuano hiyo, Diao amemtetea na kocha wa timu yake ya taifa Aliou Cisse kusalia katika nafasi yake na kuiruhusu timu kupata nafasi ya kukua pamoja kwa michuano ijayo inayotarajiwa kufanyika nchini Cameroon wakiwania kufuzu michuano ya kombe la dunia.

No comments