KAMATI za Kudumu za Bunge zitaanza vikao vyake Jumatatu, Januari 16 hadi 29, mwaka huu
KAMATI za Kudumu za Bunge zitaanza vikao vyake Jumatatu, Januari 16 hadi 29, mwaka huu, mjini Dodoma.
Taarifa ya Bunge iliyotolewa jana mjini hapa na Kitengo cha Hahari, Elimu na Mawasiliano kwa vyombo vya habari, inaonesha kwamba, vikao hivyo vitafanyika kwa mujibu wa utekelezaji wa majukumu ya kamati hizo, kabla ya kuanza Mkutano wa Sita wa Bunge, Januari 31, mwaka huu.
Wabunge wote wanatakiwa kuwasili mjini hapa, Januari, 15, mwaka huu, tayari kwa kuanza vikao kamati hizo siku inayofuata.
Katika kipindi cha vikao hivyo, kamati 12 za wabunge zitafanya ziara, kati ya Januari 17 hadi 21, mwaka huu, kukagua miradi ya maendeleo nchini inayotekelezwa na wizara au idara zinazosimamiwa na kamati husika kabla ya kamati hizo kuendelea na vikao, Januari 23, mwaka huu.
Katika kipindi hicho, Kamati mbili za kisekta zitajadili miswada mitatu ya sheria; Kamati ya kwanza ni ya Katiba na Sheria ambayo itajadili muswada wa sheria za marekebisho ya sheria mbalimbali namba 4 wa mwaka 2016 na muswada wa sheria wa huduma ya msaada wa kisheria ya mwaka 2016.
Post a Comment