Manny Pacquiao kukabiliana na Jessie Vargas Novemba
4
Mwanandondi Manny Pacquiao atarejea ulingoni mnamo tarehe 5 Novemba kukabiliana na bingwa wa dunia wa uzani wa welter Jessie Vargas kutoka Marekani
Pacquiao, 37, bingwa wa zamani wa dunia, ametangaza kwamba atarejea licha yake kutangaza kwamba angestaafu baada ya kumshinda Timothy Bradley mwezi Aprili.
Promota wake Bob Arum alisema mwezi uliopita kwamba mwanabondia huyo kutoka Ufilipino angepigana tena mwaka huu.
"Maisha ya kustaafu hayamfai Manny kwa sasa," smeneja wa Pacquiao Michael Koncz aliambia gazeti la Los Angeles Times.
"Ndondi zimo kwenye damu yake."
Pacquiao na kundi lake watakutana 10 Agosti mjini Manila kuamua iwapo pambano hilo dhidi ya Vargas, 27, litaandaliwa Los Angeles au Dubai.
Pacquiao alishinda uchaguzi wa useneta Ufilipino mwezi Mei.
Vargas alitwaa ubingwa mwezi Machi baada ya kushinda raia mwenzake Sadam Ali.
Post a Comment