Header Ads

WASANII WA MUZI WAFARIKI DUNIA KATIKA TUKIO LA UJAMBAZI TANGA


wOLPER
Ulimwengu wa muziki na filamu wiki hii ulitawaliwa na majonzi baada ya kuwapoteza wasanii wawili wa muziki ‘Ude Ude’ na ‘Iqu’ katika tukio la kijambazi huko mkoani Tanga.
wOLPER
Wolper akimtuza Ude Ude enzi za uhai wake

Mmoja kati ya wasanii wa filamu ambao wameguzwa na tukio hilo ni Jacqueline Wolper ambapo aliingiwa na mzuka na kuamua kuandika stori ya filamu.

“R.I.P wanangu dah! siku ya leo nimejua kulia kwa kilugha walah maumivu leo ni makubwa kuliko furaha nimejikuta paka naandika stori na sasa hivi ni saa 8 usiku na bado naandika naamini siku naicheza uhusika nitauvaa machozi niliojiloanisha basi yatahusika kwenye stori na itafundisha nakulenga wahusika,” alindika Wolper kupitia instagram.
Aliongeza,“Ewe Mwenyezi Mungu tulinde jamani na utupe moyo wasubraa Inshallah. Naumia jamani siku moja misiba 3, Duh majaribu nimazito unaweza kukufuru,”
Pia msanii wa kike wa muziki, Vanessa Mdee alionyesha kusikitishwa na tukio hilo huku adai ‘Ude Ude’ kabla ya kifo chake alikuwa akimcheki kwa ajili ya kumuandikia wimbo.

No comments