Ndege ya Emirates yaanguka ikitua kwenye uwanja wa ndege Dubai, ilikuwa na watu 300
KALI ZOTE BLOG
Ndege ya shirika la Emirates kutoka India, imetua na kuanguka kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dubai ikiwa na watu 300.
Picha zilizowekwa mtandaoni zimeonesha moshi mzito mweusi ukitoka kwenye ndege hiyo bila kuonesha matairi yake ya kutulia. Serikali ya Dubai imesema abiria wote walitolewa salama na hakuna majeruhi.
Imesema shughuli za ndege kuwasili na kuondoka kumesitishwa hadi itakapotangazwa.
Ndege hiyo, Boeing 777 ilikuwa ikiingia Dubai kutoka jimbo la kusini la India, Kerala. Kulikuwa na abiria 282, wafanyakazi wa ndege 18 kutoka mataifa 20.
Post a Comment