Header Ads

Akatwa mikono kwa 'kukosa kushika mimba' Kenya

KALI ZOTE BLOG

Image captionMwanamke aliyekatwa mikono na mumewe nchini Kenya
Mwanamume mmoja nchini Kenya amedaiwa kumkata mikono yote miwili mkewe wa miaka saba kwa kutumia kisu kikubwa kwa kushindwa kumzalia watoto,katika kile kinasemekana ni kisa kibaya zaidi cha ugomvi wa nyumbani.
Mikono ya Jackline Mwende kutoka kijiji cha Kathama ,Masii katika kaunti ya Machakos ilikatwa kutoka katika kifundo cha mkono na mumewe Stephen Ngila Thenge tarehe 24 mwezi Julai.
Pia ana majeraha katika kichwa chake na shingo kutokana na shambulio hilo.
Ndugu zake wanasema kuwa wanandoa hao walikuwa na matatizo na kwamba bi Mwende alitaka kumwacha mumewe,lakini akashauriwa kutofanya hivyo na kiongozi mmoja wa dini.
Mwende anasema kuwa kabla ya shambulio hilo walikuwa wakiishi mbalimbali na mumewe kwa takriban miezi mitatu kwa kosa la kutopata watoto.
''Sijui kwa nini aikuwa akinilaumu licha ya sisi sote kwenda hospitalini mwaka uliopita na kwamba daktari alisema kuwa ni yeye aliyekuwa na tatizo la kuzaa ambalo linaweza kurekebishwa''.
Anasema kuwa mumewe ambaye ni mshonaji nguo katika mji wa Masii alikataa kufuatilia matibabu.

No comments