Header Ads

Awamu ya pili ya utoaji wa vitambulisho vya taifa imeanza kwa baadhi ya wabunge


Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa NIDA - ROSE MDAMI akiwaeleza wabunge
 Awamu ya pili ya utoaji wa vitambulisho vya taifa imeanza kwa baadhi ya wabunge na wafanyakazi wa Bunge kupokea vitambulisho hivyo baada ya vile vya awamu ya kwanza kubainika kuwa na mapungufu.

Akizunguza baada ya kupokea kitambulisho chake, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi MWIGULU  NCHEMBA amewataka watanzania kujitokeza kupata vitambulisho vipya vilivyoboreshwa.

Kwa upande wake Mbunge wa Mikumi JOSEPH HAULE Ameshauri  vitambulisho hivyo vijumuishe matumizi mbalimbali.

Naye Kaimu Mkurugenzi wa kitengo cha Mawasiliano Mamlaka ya Vitambulisho vya taifa NIDA -  ROSE MDAMI amesema zoezi hilo limepangwa kufanyika kwa awamu.

Uandikishaji kwa ajili ya vitambulisho unatumia mashine za kielektroniki zilizotumika wakati wa uandikishaji wa wapiga kura kwa ajili ya uchaguzi Mkuu uliopita.

No comments