Mapigano kusitishwa saa nyingine 48 nchini Syria
Wizara ya mambo ya
ndani ya Marekani imesema kuwa Washington na Moscow wamekubaliana
kusitisha mapigano saa nyingine 48. Usitishwaji huo uliondaliwa na nchi
hizo mbili umeleta matokeo kwa siku mbili na waangalizi wanasema kuwa
hakuna watu waliokufa ndani ya siku hizo licha ya kuwepo kwa vurugu
kadhaa.
Katibu mkuu wa umoja wa mataifa Ban Ki-moon amesema kuwa
kukosekana kwa maandalizi ya kiusalama bado kuna kwamisha misaada ya
kibinadamu.
Ameongeza kuwa aliiomba Moscow na Washington kushirikiana na washirika wao ili kuhakikisha misaada inafika kwa wakati.
Uondoaji wa vikosi vya waasi na serikali katika maeneo ya barabara muhimu unatarajiwa kuanza leo.
Umoja
wa mataifa bado hawajaweza kupeleka misaada ya kutosha ya kibinadamu
katika maeneo yaliyozingirwa huko Syria, hususani katika maeneo
yanashikiliwa na waasi Mashariki mwa Aleppo licha ya kusitishwa kwa
mapigano.
Magari ya Urusi yamefika maeneo yanayoshikiliwa na serikali huko jimbo la Homs.
Wanasiasa
wapinzani wanasema kuwa serikali ya Syria ilisisitiza kusambaza na
kusimamia misaada hali inayozuia usambazaji wake, lakini mwandishi wa
BBC amesema kuwa haja ya kupata usalama kutoka kwa makundi ya waasi nayo
inachingia ucheleweshaji huo.
Msafara wa magari ya misaada ya umoja wa mataifa unasubiri kupewa ruhusa ya kupita katika mpaka wa Uturuki kuingia Aleppo.
Carsten Hansen anatoka baraza la wakimbizi la Norway, wameweza kusambaza misaada katika baadhi ya meoneo nchini Syria.
Post a Comment