Nyota mpya mlemavu wa Afrika Kusini aibuka
Nyota mpya mlemavu wa Afrika Kusini aibuka
Mwanariadha
mlemavu wa Afrika Kusini Mahlangu Ntando, 14, ameibuka kuwa nyota mpya
kutoka kwa michezo ya Olimpiki ya walemavu inayoendelea mjini Rio,
Brazil.
Kijana huyo alishinda nishani ya fedha katika mbio za mita 200 kwa walemavu waliokatwa miguu yao juu ya magoti.
Kwa mujibu wa tovuti ya jarida la Runners World, kijana huyo alijua kutembea miaka minne iliyopita.
Ntando alimaliza na muda wa sekunde 23.77 nyuma ya Mwingereza Richard Whithead (23.39).
Afrika
Kusini awali ilijivunia nyota mlemavu Oscar Pistorius ambaye alifungwa
jela miaka sita baada ya kupatikana na hatia ya kumuua mpenzi wake Reeva
Steenkamp kwa kumpiga risasi mara nne Februari 2013.
Ntando
amefurahia ufanisi wake: "Sikutarajia ningeshinda nishani lakini nilijua
kwamba nikifanya vyema kabisa ningekuwa katika nafasi nzuri."
"Najihisi
vyema sana na ningependa kuwashukuru raia wa Afrika Kusini kwa kunipa
fursa hii. Shukrani sana kwa wote walionisaidia kufika hapa."
Post a Comment