Header Ads

halmashauri ya wilaya ya KISHAPU mkoani SHINYANGA wameiomba Serikali kusaidia mradi wa maji

halmashauri ya wilaya ya KISHAPU mkoani SHINYANGA wameiomba Serikali kusaidia mradi wa maji 

Baadhi ya wakazi wa kijiji cha UBATA katika halmashauri ya wilaya ya KISHAPU mkoani SHINYANGA wameiomba Serikali kusaidia mradi wa maji ya ziwa viktoria ikiwa ni njia mojawapo ya kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji safi katika vijiji mbalimbali wilayani humo.

 Wakizungumza katika uzinduzi wa mradi wa visima vya maji katika kijiji hicho wakazi hao wamesema ingawa badhi ya vijiji vina visima vifupi na virefu vya maji, lakini visima hivyo havitoshelezi kutokana na hali ya hewa ya wilaya hiyo ambayo ina ukame katika kipindi kirefu cha mwaka.

Kufuatia hali hiyo, Shirika lisilokuwa la Kiserikali la TCRS likakabidhi visima vya maji safi katika kijiji hicho ili kukabiliana na tatizo la uhaba wa maji katika kijiji hicho na vijiji jirani.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya visima hivyo, afisa Miradi Mwandamizi wa Shirika hilo MARY MOSHA amewaomba wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka ndani na nje ya wilaya hiyo, kuunganisga nguvu za pamoja ili kutatua kero ya maji ambayo imekuwa ikiongezek wilayani KISHAPU kutokana na mbadiliko ya hali ya hewa.

No comments