Header Ads

Imebainika kuwa video ya ile ngoma ya KAZI KAZI ya Profesa Jay na Sholo Mwamba ilitawaliwa na mabalaa makubwa na ya aina yake.

Imebainika kuwa video ya ile ngoma ya KAZI KAZI ya Profesa Jay na Sholo Mwamba ilitawaliwa na mabalaa makubwa na ya aina yake.






Video hiyo ilifanyika katika maeneo ya Uwanja wa Fisi na balaa lilianza baada ya kuanza ku'shoot', imeelezwa kuwa kulimiminika mamia ya watu, kitendo kilichompa presha Profesa kujiuliza kama atatikiwa kuwalipa watu wote wale au itakuwaje! maana walionesha kujishughulisha mno na video hiyo.
Kwa upande wake Sholo Mwamba alisema "Watu waliojaa kwenye ile video walikuja tu kwa mapenzi yao kwangu na Prof. Jay, lakini Profesa Jay alistuka sana baada ya kuona watu wanaanza kucheza na mapanga na zile silaha nyingine nyingi unazoziona".
Pia akaongeza "Sehemu nyingine iliyoleta ugumu zaidi, ni pale unapoona watu wanacheza kamari, kulitokea vurugu kubwa, wahuni walipigana sana".
Akizungumza na eNewz, Sholo Mwamba aliomba wadau wa muziki waendelee kutoa support kubwa kuukuza muziki wa Singeli.
Pia akatumia nafasi hiyo kuweka wazi kwamba kwa sasa anafanya kazi chini ya usimamizi Endless Fame ya Wema Sepetu.

No comments