Header Ads

Chelsea, Wilaya ya Manhatan watu 29 wamejeruhiwa.

Mlipuko umetokea jijini New York, katika eneo la Chelsea, Wilaya ya Manhatan  watu 29 wamejeruhiwa.

Mlipuko mjini New York


Hakuna mtu ye yote aliyepata majeraha ya kuhatarisha maisha yake.
Polisi wanashuku huenda mlipuko huo ulisababishwa na kifaa cha kilipuzi na wanaendelea na uchunguzi kubaini ukweli wa mambo.
Meya wa New York, Bill de Blasio amesema mlipuko huo ulisababishwa kimakusudi lakini akasisitiza kuwa hadi sasa haujahusishwa na kundi lolote la kigaidi.
Amesema pia kuwa hakuna ushahidi kuwa mlipuko huo una uhusiano wowote na bomu la mfereji lililolipuka katika jimbo jirani la New Jersy saa chache zilizopika.
Bomu hilo lililipuka karibu na mahali ambapo mbio za kukusanya pesa za kuwasaidia wanajeshi wa zamani zilikuwa zikiendeshwa.
Hakuna mtu aliyejeruhiwa.

No comments