Profesa Lipumba awaumiza vichwa wa somi
JUMUIYA ya Vyuo Vikuu ya Chama cha Wananchi (CUF) tawi la Chuo Kikuu
cha Dar es Salaam (UDSM), imemshauri aliyekuwa Mwenyekiti wa Taifa wa
chama hicho Profesa Ibrahim Lipumba kuachana na chama hicho.
Taarifa iliyotolewa leo na Mwenyekiti wa jumuiya hiyo, Jidawi Chande
imesema kuna mpango wa kuvuruga chama hicho unaofanywa na Profesa
Lipumba na kumuonya kuacha kujidhalilisha na kujishushia heshima
aliyojijengea miaka mingi katika jamii ya ndani na nje ya nchi.
Iliongeza kuwa anachokifanya Profesa Lipumba, si tu kwamba
anajidhalilisha au kujifedhehesha tu, bali anaidhalilisha jamii nzima ya
wasomi wenye hadhi kama yeye.
“Inasikitisha sana kuona mtu kama Profesa Lipumba aliyewahi kushika
wadhifa wa uenyekiti wa chama Taifa, leo anakuwa mstari wa mbele
kukivuruga na kukigawa chama.Tunamtaka Lipumba aheshimu maamuzi halali
ya chama na afuate Katiba kwa maslahi ya chama na si kwa maslahi yake
binafsi,” amesema.
Taarifa hiyo pia imelaani fujo na kauli za kibaguzi, zinazoendelea
kutolewa na Profesa Lipumba na baadhi ya wafuasi wake, kama ya aliyekuwa
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Tanzania Bara, Magdalena Sakaya kuwa chama
kina mpasuko wa Bara na Visiwani.
Taarifa hiyo pia imeliomba Baraza Kuu na mamlaka nyingine za chama
hicho, kuendelea kufanya uamuzi mgumu ya kukijenga chama pale inapobidi,
kwani misingi na taratibu za chama lazima zifuatwe.
Post a Comment