Header Ads

Mashirika ya misaada yanatarajia kuanza kutoa misaada ya dharura haraka sana katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria.

KALI ZOTE BLOG
Moja ya eneo lililoathirika na vita Syria
Mashirika ya misaada yanatarajia kuanza kutoa misaada ya dharura haraka sana katika maeneo yaliyozingirwa nchini Syria.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi amesema kuwa misaada ya kibinaadamu itapelekwa haraka huko Alepo ambapo vikosi vinavyounga mkono serikali vilitekwa hivi karibuni.
Moja ya eneo lililoathirika na vita Syria
Image captionMoja ya eneo lililoathirika na vita Syria
Usitishwaji wa mapigano ndani ya masaa 48 unatarijiwa kuhakikisha upatikani wa misaada kwa maeneo yaliyozingirwa.
Waziri wa mambo ya nje wa Marekani John Kerry ameielezea hali hiyo kuwa ndio nafasi pekee ya kuleta amani nchini Syria.
Amesema kuwa Urusi wameahidi kuwa Rais Assad ataheshimu makubaliano hayo.
Zaidi ya watu 2,000 wameuawa katika mapigano ya siku 40 mjini Aleppo
Image captionZaidi ya watu 2,000 wameuawa katika mapigano ya siku 40 mjini Aleppo
Wanaharakati wamesema kuwa usitishwaji wa mapigano unahitajika haraka iwezekanavyo.
Mkazi wa sehemu ya mashariki mwa Alepo kunakoshikiliwa na waasi ameiambia BBC kuwa mapigano yaliyokua yanaendelea yamesitishwa na hakuna tena ndege katika anga la mji huo.
Jeshi la Syria limesema kuwa makubaliano hayo yatadumu kwa siku saba lakini bado wana haki ya kujibu ukiwaukwaji wowote kutoka kwa makundi ya waasi.

No comments