Header Ads

shilole na nuh mziwanda wawili hawa wamepostiana Instagram


Wasanii wa bongofleva Shilole na Nuh Mziwanda waliwahi kuwa wapenzi lakini wakaachana na baada ya hapo Shilole alionekana kutotaka hata kusamiliana na Nuh japokua walifikia kupatanishwa.


Banda ya haya yote September 15/9/ 2016 wawili hawa wamepostiana Instagram kwa mara ya kwanza toka kuachana kwao,


Ilikuwa ni ‘break up’ iliyofuatiwa na uadui mkubwa. Ilipelekea hadi Nuh Mziwanda kuandika wimbo ‘Jike Shupa’ uliomlenga ex wake Shilole.
nuih
Haikuishia hapo, wawili hao waliendelea kurushiana maneno kwenye mitandao ya kijamii na kwenye mahojiano na kulaumiana kwa mengi. Hata hivyo mlalamikaji mkubwa alikuwa Nuh aliyemwelezea Shishi kama mwanamke aliyempotezea muda wake na kumkwamisha kwenye muziki.
Pia wimbo wa Shilole, Say My Name una mashairi yanayotaka kuhusiana na vunjiko la huba kati ya mastaa hao waliotengeneza vichwa vya habari wakiwa pamoja ikiwa ni pamoja na kujichora tattoo za majina yao.
Na sasa huenda wameamua kuyaacha yaliyopita yapite na wagange yajayo. Alhamis hii wawili hao waliweka picha zao kwenye Instagram kwa mara ya kwanza tangu waachane.
shishi
Akiweka picha ya Nuh kwenye akaunti yake ya Instagram, Shilole aliandika: God Bless You.

shishi-2
Naye Nuh alimweka Shishi kwenye akaunti yake na kuandika: Nakutakia kila la kheri mwanangu Mungu akuzidishie uendelee kutoboa katika Kazi yako.”


No comments