Kwa Blac Chyna, hicho ndicho amesema atakifanya.. kula kondo la nyuma (placenta) pindi akijifungua
Kwa Blac Chyna, hicho ndicho amesema atakifanya.. kula kondo la nyuma
(placenta) pindi akijifungua mtoto wake aliyempata na Rob Kardashian.
Model huyo mwenye miaka 28, ameuelezea mpango wake kwenye podcast ya
Play.It’s Loveline with Amber Rose Jumatano hii. “Najisikia kuwa kwa
mtoto wangu wa pili, nimeelimika zaidi kuliko wa kwanza,” Chyna
alimweleza rafiki yake, Rose, 32.
“Ninasoma faida za kumnyonyesha mtoto wako, na hivi karibuni
nimejifunza kuhusu vitu vipya, kuhusu kutokata kondo la uzazi. Kama
umebaini, mbwa na paka, wanapozaa watoto wao, hula kondo la nyuma.
Utasema hapa usifanye hivyo, lakini hufanya, na ni kitu cha afya,”
alisisitiza.
Kula kondo la nyuma si kitu kigeni hata hivyo katika nchi mbalimbali.
Kondo la nyuma ni ogani inayojishikilia katika ukuta wa nyumba ya uzazi
ambayo huunganika na kitovu cha mama na hivyo huwa kama daraja
linalomuunganisha mama na mtoto kabla hajazaliwa.
Hufanya kazi ya kusafisha hewa safi, damu, huchuja chakula na kukitoa
kwa mama kwenda kwa mtoto na kazi zingine. Baada ya mama kujifunza,
hutupwa na huwa halina kazi tena. Lakini wengine hulichukua na
kulikaanga na kula kama nyama na wengine hulikausha na kutengeneza
vidonge na pia wapo wanaolila likiwa bichi hivyo hivyo mara tu baada ya
kutoka tumboni kwa mama.
Post a Comment